Walinda amani wa Umoja wa Mataifa na wakazi wa Timbuktu nchini Mali wanachanganya udongo ili kukarabati msikiti wa Djingareyber ulio kwenye orodha ya urithi wa dunia. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Wakazi wa Timbuktu kwa pamoja wanachanganya vizuri udongo tayari kuanza kazi. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Dua inahusika kwa msikiti huu wa Djingareyber uliojengwa mwaka 1325. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Wanapokezana udongo huu ambao utatumika kwenye ukarabati wa msikiti. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Kwa karne saba sasa kila mwaka msaragambo hufanyika ili kuuimarisha. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Licha ya mapigano huko huko Timbuktu, ukarabati huu huwaleta wanajamii pamoja. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)
Wazee kwa vijana… haba na haba hadi kazi nakamilika. (Picha: @MINUSMA-Tiecoura N’DAOU)